Dodoma FM

Miradi ya serikali iwanufaishe wananchi wa kawaida

6 August 2024, 5:50 pm

Picha ni Madiwani ambao walikuwa katika kikao cha taarifa ya mwaka.Picha na Mariam Kasawa.

Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji ambapo kilikuwa kikao cha taarifa cha mwaka na kuhudhuliwa na madiwani kutoka kata za jiji la Dodoma.

Na Mariam Kasawa.
Viongozi wametakiwa kuhakikisha miradi inayo anzishwa na serikali inawapatia fursa na kuwasaidia wananchi hususani wananchi wa kawaida.

Hayo yamesemwa na mstahiki meya wa jiji la Dodoma . Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa katika kikao cha taarifa cha mwaka katika balaza la Madiwani ambapo amesema wananchi wa kawaida watizamwe na viongozi hawa jinsi watakavyo weza kuzitumia fursa hizo.

Sauti ya Prof. Davis Mwamfupe.
Picha ni mstahiki meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe.Picha na Mariam Kasawa.

Aidha Prof. Mwamfupe amesema kwasasa wanafunzi wa wanao jifunza kwa njia ya vitendo wapo katika ofisi mbalimbali hivyo amesema wapangiwe kutembelea maeneo ya kata ili wajifunze na kufahamu chaangamoto za wananchi kuliko kushinda ofisini wakati mwingine bila kazi.

Sauti ya Prof. Davis Mwamfupe.

Nae Diwani wa kata ya Ipagala Mh. Doto Gombo pamoja na Naibu meya walikuwa na haya yakusema katika kikao hicho.

Sauti ya Naibu meya na Diwani wa kata ya Ipagala.