Uwezeshaji wanawake ni chachu ya kuwainua kiuchumi
6 August 2024, 5:04 pm
Uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi ni muhimu kwa haki za Wanawake, kwa Ustawi, Ushawishi, Mamlaka, na usawa wao.
Na Fred Cheti.
Uwezeshaji Wanawake kiuchumi unaofanywa na Serikali, Wadau, pamoja na Familia, unatajwa kuwa moja ya chachu inayoweza kuwainua Wanawake kimaendeleo katika Jamii.
Hayo yameelezwa na mmoja wa Wanawake ambae ni Mjasiriamali Devotha Felex ambae amewezeshwa na mwenza wake katika Biashara zake ambapo amesema jambo hilo limemuinua kwa kiasi kikubwa.
Dodoma TV imepita Mtaani kuzungumza na baadhi Wananchi kuhusu umuhimu wa kuwawezesha Wanawake katika nyanja zote za kiuchumi ambao walikuwa na haya ya kueleza.
Uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi ni muhimu kwa haki za Wanawake, kwa Ustawi, Ushawishi, Mamlaka, na usawa wao, pia kwa mafanikio ya Biashara na uchumi. Katika Nchi zenye uchumi wa kiwango cha chini na cha wastani, Wanawake wanafanya kazi nyingi za huduma za Matibabu na kazi za Nyumbani, na wanatoa huduma ya Matibabu ya muda mrefu bila malipo