Dodoma FM

Taka rejeshi zatajwa kuwanufaisha kiuchumi baadhi ya wananchi

2 August 2024, 5:45 pm

Picha ni taka aina ya chupa mbalimbali zikiwa zimezagaa kwenye mazingira.Picha na George John.

Kumekuwa na marundo mbalimbali ya taka kama chupa za plastiki, makaratasi, chuma, chupa, taka ambazo zinaweza kurejeleshwa na kutumika katka matumizi mengine mbadala na zikaleta faida.

Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kutambua kuwa taka rejeshi zikitumika ipasavyo zinaweza kusaidia watu wengi kujikwamua kiuchumi.

Katika mazingira tunayoishi, sehemu tunazofanya kazi hata njiani tunapopita tunakutana na taka mbalimbali ambavyo huzalishwa na kutupwa huku watu wengi wakiamini taka hizo hazina thamani tena.
Wajasiriamali wanaojihusisha na uokotaji na uuzaji wa chupa za plastiki wanasema biashara hii imekuwa msaada kwao japo wakati mwingine soko la chupa linakuwa gumu lakini kwa kiasi kikubwa biashara hii imeweza kuwainua kiuchumi.

Sauti za wanunuzi wa chupa.
Picha ni utangenezaji wa mkaa mbadala unaotokana na karatasi.Picha na Mariam Kasawa.

Happy Mushi ni binti anayejihusisha na uuzaji wa mkaa mbadala unao tengenezwa na karatasi yeye anasema vijana wanapaswa kujifunza na kuwa wabunifu katika mazingira hasa katika uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na taka rejeshi ambazo hazihitaji mtaji mkubwa kuifanya.

Sauti ya Happy Mushi.