Kusuasua kwa huduma ya maji kero kwa wakazi wa mtaa wa Miganga
2 August 2024, 5:26 pm
Mhandisi Aron Joseph anasema bado hawajaweza kufikia 100% ya malengo ya utoaji wa huduma za maji Dodoma lakini mpaka mwisho wa mwaka wa fedha wa 2024/25 watafikia 75%.
Na Mindi Joseph.
Kusuasua kwa upatikanaji wa huduma ya maji katika mtaa wa Miganga kata ya Mkonze mkoani Dodoma imetajwa kuwa kero kwa wakazi wa eneo.
Eneo hilo limekuwa likipata maji kwa mgao lakini wakazi hao wanasema ikifika siku ya mgao maji hayatoki na hii imekuwa ikiwalazimu kununu maji dumu 500.
Duwasa inazalisha maji asilimia 52% ya maji yanayohitajika katika mji wa Dodoma sawa na lita milion 79.1 kwa siku, huku mahitaji kwa siku moja ni lita milioni 149 na kusababisha maji kuwa ya mgao na hapa Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga Ludovick Chogwe anasema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph anasema ni kweli maji ni ya Mgao na hapa anaainisha sababu na jitihada wanazofanya kunusuru hali ya wananchi.