Dodoma FM

Tusiwachukie, tuwape watu vitu

1 August 2024, 5:33 pm

Mchungaji wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kaskazini ushirika wa Kongwa Dr Ipyana Mwangota akiwa pamoja na watu wenye uhitaji kanisani hapo. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Kanisa la Moraviani Ushirika wa Kongwa limeanzishwa mwaka 2008, ni moja ya makanisa madogo wilayani Kongwa.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Imeelezwa kuwa kuishi katika jamii isiyokuwa na upendo ni sababu kubwa inayopelekea dunia kuwa na matukio ya kikatili na mauaji kwa watu wenye ualbino na watoto.

Hayo yameelezwa na mchungaji Dkt. Ipyana Mwangota wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kaskazini ushirika wa Kongwa katika ibada kubwa ya kuwasaidia watu wasiojiweza watoto wanawake na wazee iliyofanyika kanisani hapo.

Mwangota ameeleza kuwa Mungu ndiye asili ya upendo hivyo kwa kuwa wanadamu wote tunatoka kwa Mungu tuache Tabia za kibinadamu badala yake tuwe na upendo wa kimungu tuwatendee watu mema tuwakaribishe wageni na kuwapa watu vitu hususani wenye uhitaji.

Sauti ya Dkt. Ipyana Mwangota .
Mchungaji wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kaskazini ushirika wa Kongwa Dr Ipyana Mwangota akiwa pamoja na watu wenye uhitaji kanisani hapo. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kuwa wanashukuru Mungu Kwa nafasi hiyo ambayo Mungu amewapatia ya kuwasaidia watu ni jambo jema kujumuika pamoja kwa upendo.

Sauti ya muumini wa kanisa hilo.

Akiongea kwa niaba ya watu waliopokea msaada huo bi Matha Mchome ameshukuru uongozi wa kanisa hilo kwa moyo waliouonesha wa kujali watu wengine na kuomba madhehebu mengine kuiga mfano huo ili kujenga jamii moja.

Sauti ya Bi.Martha Mchome.