Dodoma FM
NIRC yatarajia kuchimba visima 60,000 nchini
30 July 2024, 6:26 pm
Mpango huu unalenga kuwa na visima vyenye uwezo wa kuhudumia wakulima na umelenga kuinua sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Na Mindi Joseph.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kupitia Wizara ya Kilimo inatarajia kuchimba visima 60,000 nchini kwa ajili ya kuendeshea kilimo cha umwagiliaji.
Katika awamu ya kwanza visima 150 vinatarajiwa kuchimbwa na vitahudumia wakulima 16 kwa kila kisima kimoja na Tayari Tume imeanza kufanya ufuatiliaji kupitia wataalam kutoka Halmashauri zitakazonufaika na visima hivyo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Salome Mallamia katika mahojiano na Dodoma Tv.
Kwa upande wa wakulima wamezungumzia mpango huo.