Dodoma FM

Jamii yatakiwa kudumisha kampeni ya mtu ni afya

29 July 2024, 7:18 pm

Picha niAfisa Afya mkuu bi. Mariam akifanya usafi katika wa mtaa wa Mwaja katika utekelezaji wa kampeni ya mtu ni Afya.Picha na Mariam kasawa.

Ikumbukwe kuwa kampeni ya Mtu ni Afya yenye kaulimbiu inayosema Fanya kweli, Usibaki nyuma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 9 Mei, 2024 .

Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kufanya usafi katika mazingira yanayo wazunguka ili kuepukana na magonjwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Hayo yamesemwa wakati Wizara ya Afya na Halmashauri ya jiji la Dodoma walipo shirikiana na wananchi wa mtaa wa Mwaja uliopo kata ya Chamwino kufanya usafi wa mazingira.

Akiongea wakati wa usafi huo Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu amesema usafi wa mazingira uasaidia wananchi kuepukana na magonjwa hususani magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa tishio kwa jamii.

Sauti ya Dkt. Ona Machangu.

Aidha Dkt. Ona ameongeza kuwa kupitia kampeni ya Mtu ni Afya yenye vipaumbele 9 kipaumbele kimoja wapo ni kuhakikisha usafi wa mazingira unazingatiwa pamoja na kuhakikisha wananchi wanafuata kauli mbiu ya mita 5 usafi wangu, usafi wangu mita 5.

Picha ni wakazi wa mtaa wa Mwaja wakifanya usafi wa mazingira.Picha na Mariam Kasawa.

Naye Afisa Afya Mazingia Mkuu kutoka Wizara ya Afya Bi. Mariam Mashimba ameiomba jamii yote kuzingatia usafi wa mazingira katika maeneo yao wanayoishi pamoja na maeneo ya biashara zao.

Sauti ya Bi. Mariam Mashimba.

Kwa upande wa wananchi walio shiriki zoezi la usafi wameishukuru Serikali kwa kuanzisha kampeni ya Mtu ni Afya kwani itaenda kuhamasisha na kuelimisha jamii kuweza kuzingatia usafi wa mazingira yao ili kuweza kuwa na afya bora.

Sauti za wananchi.