Ukarabati shule ya msingi Michese wasaidia kupunguza utoro
24 July 2024, 5:07 pm
Shule ya Msingi Michese ina zaidi ya wanafunzi 2000, walimu wakiwa ni 40 na madarasa 16 huku ikiwa na uhitaji wa madarasa 44 ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Na Mindi Joseph.
Zaidi ya Shilingi Milioni 100 zimetumika katika Ukarabati wa Miundombinu ya Madarasa 11 katika Shule ya Msingi Michese na kuchangia kupunguza utoro kwa wanafunzi.
Madarasa haya kabla ya ukarabati yalikuwa yamechakaa na kusababisha wanafunzi kutoroka shuleni lakini jitihada mbalimbali zimefanyika kuhakikisha madarasa hayo yanakarabatiwa na kuboresha mazingira ya wanafunzi katika ujifunzaji.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani Sospiter Abel anasema kabla ya ukarabati huo wanafunzi walikuwa wachache kutokana na utoro.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mwl. Fredrick Mwakisambwe anasema serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha miumbombinu ya elimu inaboreshwa.
Diwani wa kata ya Mkonze David Bochela anabainisha kuwa milioni Mia moja zimetumika katika ukarabati wa madarasa hayo 11.