Dodoma FM

Wanawake wanashindaje vikwazo na kuwania uongozi kisiasa?

24 July 2024, 3:57 pm

Kwa kasi ya sasa ya maendeleo, uwakilishi sawa bungeni hautafikiwa hadi mwaka 2062.Picha na BBC

Japo hivi sasa tunajikongoja licha bado juhudi zinahitajika ili usawa na sauti ya pamoja zisikike kwenye mabaraza ya Maamuzi kuanzia ngazi ya mtaa/kijiji hadi kitaifa.

Na Seleman Kodima.
Ifahamike kuwa ulimwenguni Katika nchi 193 wanachama wa Umoja wa MAtaifa, ni nchi na serikali 28 tu ndio zinaongozwa na wanawake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, kwa kasi ya sasa ya maendeleo, uwakilishi sawa bungeni hautafikiwa hadi mwaka 2062.

Hapa nchini Tanzania Takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 1995, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanza idadi ya wanawake waliokuwa wakijitokeza kuwania uongozi kwenye uchaguzi mkuu ilikuwa ndogo.

Kutokana na hilo Mwenzetu Selemani Kodima ametuandalia taarifa ifuatayo kuhusu Diwani wa kata ya Mbabala ambaye ni Mwanamke alivishinda vikwazo na kuwania nafasi hiyo ya Uongozi wa kisiasa.