Serikali yaombwa kuendelea kutoa elimu matumizi ya nishati safi
23 July 2024, 4:04 pm
Umuhimu wa agenda ya nishati safi unasukumwa na ongezeko la uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi pamoja na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wameiomba serikali iendelee kutoa elimu juu ya matumizi ya nishati safi pamoja na kupunguza bei ya gesi ili waweze kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Wakiongea na Dodoma Tv wakazi wa mtaa wa Swaswa uliopo kata ya Ipagala Jijini Dodoma wanasema wanatamani kuzifahamu nishati zingine ikiwemo makaa ya mawe lakini upatikanaji wake sio rahisi.
Aidha wananchi hao wanaiomba serikali iendelee kupunguza bei ya gesi ili watu wenye kipato cha chini wamudu kutumia nishati hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Swaswa Bw. Charles Nyuma anasema wanaendelea kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi licha ya wananchi wengi kulalamika kuwa nishati safi ina gharama.
Bw. Charles Nyuma ameiomba serikali iendelee kushusha gharama za gesi.