Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwahimiza watoto kusoma

23 July 2024, 3:49 pm

Picha ni Diwani wa kata ya Mkonze Mh David Bochela wakati akizungumza na Dodoma Tv.Picha na George John.

Hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na viongozi wa kata ya Mkonze kuhakikisha watoto wanapofauli wanazingatia masomo.

Na Mindi Joseph.

Wazazi wametakiwa kujali misingi ya watoto kwa kuwahimiza kusoma na kuwalea katika mazingira ya kufanya vizuri katika taaluma.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Mkonze Mh. David Bochela wakati akizungumza na Dodoma Tv anasema serikali inawekeza pesa nyingi kwenye elimu hivyo wazazi wanajibu wa kuhakikishi watoto wanasoma.

Sauti ya Mh. David Bochela.
Picha ni wanafunzi wakiwa katika moja shule mpya ambayo imeanza kutumika.Picha na George John.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani Sospeter Abel Masweta anasema moja ya changamoto inayojitokeza ni watoto wanapofaulu kukataa kusoma na wazazi kushindwa kuwajibika.

Sauti ya Bw.Sospeter Abel Masweta .

Wazazi ndio wanatupiwa lawama kushindwa kuwajibika na nimezungumza na baadhi ya wazazi kufahamu pindi mtoto anapofaulu na kukataa kusoma wanawajibikaje.

Sauti za Wazazi.