Wananchi waaswa kuwakacha viongozi watoa rushwa kwenye uchaguzi
22 July 2024, 6:54 pm
Rushwa ni chanzo cha kupatikana kwa viongozi wasio na maadili.
Na Fred Cheti.
Ikiwa Tanzania inatazamiwa kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani rushwa imekuwa ikitajwa kama moja ya kikwazo kinachangia kupatika kwa Viongozi wasio wazalendo na waadilfu.
Dodoma Tv imepita mtaani na kuzungumza na baadhi ya Wananchi kuhoji je wanafahamu madhara ya kumchagua kiongozi anayetumia fedha au vitu vingine ili aweze kupata kura katika uchaguzi?
Viongozi mbalimbali wamekuwa wanasisitiza Wananchi kuacha tabia ya kuwachagua Viongozi wanaotumia rushwa ili wachaguliwe kama ambavyo anazungumza Waziri mkuu mstaafu katika Serikali ya awamu ya nne Mizengo Pinda
Kwa Mujibu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa Nchini (TAKUKURU) rushwa ni chanzo cha kupatikana kwa Viongozi wasio na maadili, wasio zingatia misingi ya haki, usawa, uwazi, uwajibikaji na uzalendo, pia Taasisi hiyo inaongeza kuwa rushwa imekuwa ikidhoofisha Utawala bora na Demokrasia Nchini kwa Wananchi wenye sifa za uongozi kushindwa kugombea au kuteuliwa kutokana na kutokua tayari kutoa rushwa.