Miundombinu bora ya shule yaongeza kiwango cha ufaulu Lukundo Sekondari
22 July 2024, 5:59 pm
Shule ya Sekondari Lukundo imeendelea kushika nafasi ya 2 ki Wilaya na 3 bora kwa Mkoa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).
Na Mindi Joseph.
Uboreshaji wa Miundombinu ya Wanafunzi na Walimu kwa shule ya Lukundo Sekondari imeendelea kuongeza viwango vya ufaulu kwa Wanafunzi kwa miaka mitatu mfululizo.
Shule hii iliyopo katika Kata ya Chang’ombe Mkoani Dodoma ina asilimia 92 ya ubora wa Miundombinu ya Wanafunzi na kuendelea kuiweka katika matokeo mazuri ya ufaulu ikishika nafasi ya 2 kwa Wilaya katika Mkoa wa Dodoma Kwa mujibu wa matokeo ya Baraza la Mitihani Tanzania NECTA ikichuana vikali na shule za binafsi.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Lukundo Sekondari Asafu Thadeo Makonda amezungumza na Dodoma Tv.
Wanafunzi wanaamini uboreshaji wa miundombinu ya Walimu ya kufundishia ndio imeogeza ufaulu kwao.
Shule hii imekuwa ikitazamwa kwa ukaribu na Viongozi ikiwemo Diwani wa Kata ya Changombe Bakari Fundikila kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo viti 20 na madawati 20 ya Walimu.
Afisa Elimu Kata ya Changombe Rebecca Haule anaeleza hali ya Elimu katika Kata yake huku akiwapongeza Walimu.