Dodoma FM

Mila, desturi kikwazo wanawake kuwania nafasi za uongozi

19 July 2024, 4:20 pm

Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi. Picha na Michuzi blog.

Takwimu zinaonesha bado hakuna uwakilishi wa kutosha wa wanawake katika nafasi za uongozi, za kuchaguliwa au kuteuliwa katika ngazi mbalimbali za uongozi na hata hivyo ukilinganisha na tulipotoka, kuna mabadiliko chanya katika ushiriki wa wanawake na uongozi.

Na Alfred Bulahya
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu, imeelezwa kuwa mila na desturi bado ni changamoto zinazowakwamisha wanawake kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa kiasiasa.

Kufahamu zaidi kuhusu hilo tuungane na mwandishi wetu Alfred Bulahya ambaye yeye amezungumza na Afisa Jamii kutoka Taasisi ya Vijana Tanzania Sarafina inayojihusisha na utoaji wa elimu ya uongozi kwa vijana jijini Dodoma.