Wilaya ya Bahi yafikia malengo ukusanyaji wa mazao ya chakula
17 July 2024, 4:42 pm
Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Nchini TANIPAC unalenga kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula hususani mahindi na karanga na kusaidia kuimarisha usalama wa chakula.
Na Kadala Komba.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma imefanikiwa kufikia lengo la kiwango sahihi cha ukusanyaji wa mazao kwa ajili ya uwepo wa hifadhi ya kutosha ya chakula cha akiba.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya bahi zaina mlawa amebainisha hayo katika kongamano la utoaji elimu kwa watendaji wa kata na maafisa ugani wa halmashauri hiyo juu ya sheria ndogo ya sumukuvu huku akikiri kuwa utolewaji bure wa mbegu za mazao umechangia kuwepo kwa ongezeko hilo.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi. Margaret Natai amesema kutokana na madhara yanayotokana na vimelea vya sumukuvu Serikali ilianzisha Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu ili kutoa elimu kwa wakulima waweze kunusuru mazao yao.
Afisa Kiungo mradi wa kuthibiti sumukuvu halmashauri ya wilaya ya Bahi Hamis Mfuko amesema wilaya ya bahi ni miongoni mwa wilaya 18 zinazotekeleza mradi wa kuthibiti sumukuvu huku mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya bahi Martha Chamwela akitoa wito kwa watendaji wa kata na maafisa ugani kusimamia sheria hiyo.