Dodoma FM

Root&Shoot na wanafunzi waadhimisha maadhimisho ya Sokwe mtu

15 July 2024, 5:13 pm

Picha ni Kamishina msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Uhifadhi kutoka TANAPA Dkt Noelia Mihonga aliposhirikia mjadala wa uliondaliwa na shirika la Root & shoot.Picha na Seleman Kodima.

Maahimisho ya Sokwe mtu huadhimishwa kila july 14 Tanzania ikiwa ni moja ya nchi wanachama wa Umoja huo unao adhimisha maadhimisho hayo.

Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa sokwe mtu ni mnyama muhimu kwa Taifa letu kwani wamekuwa kivutio tosha kwa watalii wanaokuja nchini kujionea uzuri wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Kamishina msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Uhifadhi kutoka TANAPA Dkt Noelia Mihonga aliposhirikia mjadala wa uliondaliwa na shirika la Root & shoot uliobeba mada isemayo mfahamu sokwe mtu na nafasi ya kijana kuhusu uhifadhi wa Mazingira na wanyama.

Dkt Noelia ametoa wito kwa jamii kufahamu thamani ya Sokwe mtu kwa kushirikiana katika vipindi mbalimbali vinavyoandaliwa.

Sauti ya Dkt. Noelia Mihonga.

Kwa upande wake Mratibu wa Programu kutoka shirika la Root &Shoot Moses Mfuko amesema kupitia shirika hilo chini ya Muhasisi wake Jane Goodall wamekuwa chachu ya mabadiliko ya kumuhifadhi mnyama sokwe na kuyalinda mazingira.

Sauti ya Moses Mfuko .
Picha ni Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki katika mjadala huo uliondaliwa na Roots and Shoots kuhusu maadhimisho ya sokwe mtu.Picha na Seleman Kodima.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki katika mjadala huo uliondaliwa na Roots and Shoots kuhusu maadhimisho ya sokwe mtu ,wamesema wanatarajia kuwa mabalozi wema katika utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira na uhifadhi kwa vitendo.

Sauti za Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari .