Kamati ya kitaifa ya ushauri kuhusu kizazi chenye usawa yawatembelea wajasiriamali Dodoma
10 July 2024, 5:08 pm
Kamati ya kitaifa ya ushauri kuhusu utekelezaji wa programu ya kizazi chenye usawa ipo karika ziara ya siku nne ya kutembelea vikundi mbalimbali kwa Jiji la Dodoma, Dar-es-salaam na Unguja.
Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa Tanzania ndio Nchi inayofanya vizuri Barani Afrika katika utoaji wa mikopo ya asilimia kumi.
Hayo yamesemwa na Bi Beng’i Issa katibu wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kikao cha kamati ya kitaifa ya utekelezaji kuhusu kizazi chenye usawa iliyo ambatana na ziara ya kutembelea baadhi ya vikundi .
Akiongea na wanachama wa Kikundi cha winning Star kilichopo Ilazo Mbuyuni Jijini Dodoma ambao wamejikita katika ufugaji wa kuku wa mayai Bi. Beng’i amewataka akina mama hao kuweka akiba kila faida wanayo ipata katika biashara hiyo ili waweze kufikia malengo waliyo jiwekea.
Awali akisoma taarifa za kikundi hicho cha Winning Star Katibu wa Kikundi Bi Julia Malaba ameeleza mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo katika mradi huo wa ufugaji wa kuku wa mayai .
Nao wajumbe wa kamati ya kizazi chenye usawa bi Nangi Massawe na bi. Carolyin Kandus walikuwa na haya yakusema.