Dodoma FM

Umuhimu wa lishe kwa mtoto

2 July 2024, 5:52 pm

Uwepo wa utapiamlo sugu (udumavu) unadhoofisha maendeleo.Picha na Mindi Joseph.

Kwa mujibu wa utafiti wa afya ya uzazi na mtoto viashiria ya malaria Tazania mwaka 2025/16 hali ya lishe kwa watoto inaboreka tangu mwaka 1991/92 Nusu ya watoto walikuwa wamedumaa ukilinganisha na mwaka 2015/19 asilimia 34.

Na Mindi Joseph.
Kuboresha lishe ni msingi katika kufanikisha malengo yote ya Maendeleo Endelevu.
Ikumbukwe Uwepo wa utapiamlo sugu (udumavu) unadhoofisha maendeleo katika uhakika wa chakula, uboreshaji wa elimu, na afya bora ya mama na mtoto.

Kulingana na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2015-2016, takriban theluthi ya watoto wote chini ya miaka mitano wana udumavu na asilimia 14 wana upungufu wa uzito. Sababu kuu zinazoongoza kuleta utapiamlo ni ukosefu wa lishe mchanganyiko na bora kwa kila kaya, upatikanaji mbovu wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama, usafi wa mazingira), na mienendo duni ya lishe.

Wazazi wenye watoto waliona utapiamlo wengi wanasema hawana elimu ya lishe bora kila mzazi hapa anasema.

Nin nini wajibu wa Wenyeviti kuhakikisha elimu ya lishe inafika kwa wananchi wao Mwenyekiti wa kijiji cha Uhelela Amos Mayombe anaeleza.

Elimu ya lishe imekuwa ikiwafikiaje wanachi Diwani wa kata ya Bahi Augustino Ndonu anasema.

Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linasababishwa na mtoto kushindwa kupata lishe bora tangu akiwa tumboni kwa mama yake. Akina mama wajawazito pindi wanapohudhuria kliniki husisitizwa kuzingatia lishe bore ili kumuepusha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo hayo.

Kutokana na baadhi ya akina mama wajawazito kushindwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya, uelewa duni wa namna bora ya kuandaa chakula kwa ajili ya mtoto, na hali ya maisha duni inayozikabili familia nyingi nchini, Tanzania imeendelea kukabiliwa na tatizo la udumavu, huku jitihada kadhaa zikiendelea kuchukuliwa na wadau mbali mbali kwa lengo la kukabiliana na hali hiyo.
Je kuna umuhimu wa watoto kupata Lishe Bora.

Lishe bora ya mtoto akishazaliwa inaanzia kwenye maziwa ya mama pekee Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Semeni Eva Juma hapa anasema.