Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwapa elimu watoto wenye ulemavu

2 July 2024, 5:34 pm

Picha ni wakazi wa kijiji cha Uhelela kata ya Bahi wakiwa katika kikao .Picha na Mariam Kasawa.

Mratibu wa Elimu Jumuishi Bi. Jane Mgidange kutoka shirika la FPCT amewataka wazazi na walezi kutambua kuwa watoto wenye ulemavu si mzigo bali ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo wanapaswa kuthaminiwa kama watoto wengine.

Na Mariam Kasawa.
Wazazi na walezi wametakiwa kuacha mitazamo hasi dhidi ya watoto wenye ulemavu badale yake wawape nafasi ya kujifunza na kupata elimu.

Katika kijiji cha Uhelela kata ya Bahi wakazi wa eneo hilo wengi bado hawaamini kama mtoto mwenye ulemavu anaweza kusoma na kufanya vitu kama watoto wengine kama walivyo uliza maswali kwa Mratibu wa elimu Jumuishi Bi. Jane Mgidange nae akapata wasaa wa kuwajibu.

Sauti za mwananchi na Bi Jane Mgidange.
Picha ni wanafunzi wa shule ya msingi Bahi Sokoni wakiimba shairi kuhamasisha wazazi kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu. Picha na Mariam Kasawa.

Wazazi wanapaswa kutambua kuwa mtoto mwenye ulemavu akipewa na nafasi ya kusoma na kujifunza anauwezo wa kufanya vitu mbalimbali huyu ni mzazi ambae ana mtoto mwenye ulemavu na amempa nafasi ya kujifunza hapa anasimulia.

Sauti ya Mzazi.

Wanafunzi wanasema elimu jumuishi imeleta manufaa kwa wote pia inasaidia kupunguza unyaunyapaa dhidi ya watoto wenye ulemavu shuleni.

Sauti za wanafunzi.
Picha ni Mratibu wa elimu Jumuishi Bi. Jane Mgidange akiongea na wakazi wa Kijiji cha Uhelela kata ya Bahi. Picha na Mariam Kasawa.

Lakini nini mchango wa serikali kwa watoto wenye ulemavu ambao wanasajiliwa na kuanza kwenda shule Mratibu wa Elimu kata ya Bahi anafafanua zaidi.

Sauti ya Mratibu elimu kata ya Bahi.