Dodoma FM

EWURA yawaonya wauzaji holela wa mafuta

26 June 2024, 6:20 pm

Picha ni Meneja, EWURA kanda ya kati, Bi.Hawa Lweno.Picha na Mindi Joseph.

Aidha amesema kuwa , moja kati ya changamoto iliyopo ni ukosefu wa elimu kwa jamii kuhusu huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

Na Mariam Kasawa.
Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati imeonya watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uuzaji mafuta holela kwenye vidumu huku ukiwataka kuacha mara moja kwakuwa hali hiyo ni hatari kwa maisha yao.

Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Meneja, EWURA kanda ya kati, Bi.Hawa Lweno , alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya nishati na maji.
Lweno, amesema kuwa tabia ya watu kuuza mafuta holela kwenye vidumu ni hatari kwa maisha yao kwakua maeneo wanayayatumia siyo salama.

Sauti ya Bi.Hawa Lweno

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA,Bw. Titus Kaguo, amesema lengo la kikao hicho na wadau hao ni kutoa elimu kuhusu huduma wanazozitoa.

Sauti ya Bw. Titus Kaguo.
Picha ni Madiwani pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika mafunzo hayo.Picha na Mindi Joseph.

Naye Diwani wa Kata ya Mbabala Pascazia Mayala ,ametaka kuwe na sheria ya kuwabana wauza mafuta ambao baadhi yao wamekuwa wakijaza mafuta tofauti na hela wanayolipwa.

Sauti ya Mh. Paskazia Mayala.