Dodoma FM

Uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mtu

25 June 2024, 6:50 pm

Picha ni mawakili hao wakiwa katika mafunzo hayo yaliyo fanyika katika ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.Picha na Mariam Kasawa.

Kila mtu ana uhuru wa kujieleza bila kuvunja sheria za nchi kwa kufuata taratibu na kanuni za Nchi.

Mindi Joseph.
Uhuru wa kujieleza unatajwa kuwa ni haki ya kila mtu lakini watu wanapaswa kujielewa kwanza kabla ya kutumia uhuru huu bila kuleta madhara yoyote kwa jamii.

Kauli hii inafuatia mafunzo yanayotolewa kwa wanasheria kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini yanayo fanyika hapa jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na makamu wa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS Bw. Deus Nyabiri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari amesema jamii inahitaji elimu ya kutosha kuhusu uhuru wa kujieleza.

Sauti ya Bw. Deus Nyabiri .

Kwa upande wa baadhi wanasheria walio shiriki katika mafunzo hayo wao wanasema mafunzo haya ni chachu kwao kwani watafahamu mipaka ya sheria pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya uhuru wa kujieleza.

Sauti ya Mwanasheria.