Dodoma FM

Wananchi Mapinduzi waiomba serikali kuingilia kati mgogoro uchimbaji wa mchanga

14 June 2024, 12:45 pm

Korongo hilo limekuwa likiathiri zaidi shughuli za kilimo pamoja na afya za wakazi wa eneo hilo kutokana na vumbi.Picha na Fred Cheti.

Dodoma Tv itaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi sakata hilo ili kujua hatima yake kutoka na kuleta Sintofahamu katika eneo hilo.

Na Fred Cheti.

Wakazi wa mtaa wa Mapinduzi kata ya Mbabala wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa uchimbaji wa mchanga unaofanywa na Mwekezaji kutokana na madai ya kukiuka makubaliano waliyojiwekea na Mwekezaji huyo.

Dodoma Tv imefika katika mtaa huo na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambapo wamesema kuwa mbali ya mwekekezaji anayejichimba mchanga katika korongo liliopo matani hapo kukiuka makubaliano waliyojiwekea ikiwemo kuwachimbia kisima cha maji shuguli hiyo imekuwa ikiathiri zaidi shughuli za kilimo pamoja na afya za wakazi wa eneo hilo kutokana na vumbi.

Sauti za wakazi wa eneo hilo.
Picha ni eneo hilo ambalo huchimbwa mchana na mwekezaji huyo. Picha na Fred Cheti.

Dodoma Tv Imezungumza pia na Mwenyekiti wa Mtaa huo ambapo amekiri kutokuwepo kwa maelewano mazuri baina ya Mwekezaji anayejimba mchanga katika eneo hilo na wakazi wa eneo hilo ambapo amesema wameandaa mkutano wa hadhara ili kuweka makubaliano sawa baina ya Mwekezaji huyo na wananchi.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa huo.