Vijana wa miaka 13 hadi 17 kufanyiwa upimaji Mpwapwa
13 June 2024, 10:48 am
Shirika la ACTON FOR COMMUNITY CARE linatoa mafunzo kwa wakufunzi 32 kutoka kata 20 na vitongoji 25 za wilaya ya Mpwapwa.
Na Mariam Kasawa
Upimaji wa stadi za maisha kwa vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 unatajwa kusaidia vijana kujitambua , kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zao pamoja na kuishi vizuri katika jamii.
Kupitia elimu hiyo ya upimaji hirika lisilo la kiserikali la ACTON FOR COMMUNITY CARE linatoa mafunzo kwa wakufunzi 32 kutoka kata 20 na vitongoji 25 za wilaya ya Mpwapwa ili kuwawezesha kufanya utafiti kwenye kaya 15 za kila eneo la wilaya hiyo.
Bw. Peter Mhagwa ni msaidizi wa wilaya mradi wa utafiti wa stadi za maisha yeye anaeleza kwa kina lengo la mafunzo hayo kwa vijana hao 32 na nini wanakitarajia baada ya upimaji.
Nae Bw. Gerald Chanai vilaage coordineta wa mradi huu anasema tathmini hii imekuwa likisaidia zaidi husani kwa taasis za kielimu katika kubadilisha mitaala shuleni.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo haya wanasema mafunzo haya yamewapa mwanga na wamefahamu nini maana ya stadi za maisha.