Dodoma FM

DUWASA yapiga marufuku matumizi ya maji taka

10 June 2024, 6:53 pm

DUWASA wameendelea kuhakikisha maji taka yanayotibiwa hayaleti athari kwa jamii. Picha na Duwasa.

Serikali ya Awamu ya Sita imetenga shilingi Bilion 160 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa mabwawa 16 ya kutibu maji taka katika kata ya Nzuguni na mradi huu utaanza kutekelezwa mwazi July 2024.

Na Mindi Joseph.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira DUWASA imesema ni marufuku kutumia maji taka kwenye Kilimo au nyumbani kwani yana athari kiafya.

Maeneo yenye watu wengi na miji iliyoendelea hutegemea mitambo ya kati ya kutibu maji machafu kupokea na kutibu maji taka.

Picha ni Msanifu wa Ujenzi wa Majitaka DUWASA Mhandisi Aloyce Emirani.Picha na DUWASA

Maria Holela ni afisa Mazingira DUWASA anasema maji taka hayaruhusiwi katika shughuli za kibinadamu na wameendelea kuhakikisha maji taka yanayotibiwa hayaleti athari kwa jamii ikiwemo kutotumika katika Kilimo.

Sauti ya Bi. Maria Holela.

Mifumo ya Tiba ya maji taka iliyopo inafanyaje kazi na njia Zipi zinazotumiwa kutibu maji taka.
Msanifu wa Ujenzi wa Majitaka DUWASA Mhandisi Aloyce Emirani anaelezea uratibu wa maji taka kabla ya kuingia katika mabwawa.

Sauti ya Mhandisi Aloyce Emirani.