Maonesho ya siku ya mazingira yazinduliwa Jijini Dodoma
3 June 2024, 7:23 pm
Urejeshaji wa ardhi iliyo haribiwa na ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kutumia Bunifu na Teknolojia mbalimbali za utunzaji wa mazingira ili kunusuru mazingira.
Maonesho ya siku ya mazingira ambayo kitaifa yanafanyika hapa Jijini Dodoma yamezinduliwa leo na Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Mh. Dkt. Dotto Biteko ambapo amezitaka Taasisi kuendelea kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na wananchi kuendelea kujifunza kupitia bunifu na teknolojia.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Dkt Seleman Jafo anasema taasisi mbalimbali hapa nchini zimekuwa zikijibidiisha katika utunzaji wa mazingira pia na miradi ya ujenzi wa barabara imechangia kupunguza gesi joto .
Akiongea wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule amesema Mkoa umefanikiwa kwa asilimia 70 katika kampeni ya soma na mti pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji likiwemo bonde la makutupora
Maonesho ya siku ya mazingira Duniani ambayo yamezinduliwa leo yatahitimishwa juni 5 ambapo kitaifa yanafanyika hapa Jijini Dodoma huku yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Urejeshaji wa ardhi iliyo haribiwa na ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame.