Dodoma FM

Kilimo cha umwagiliaji mkombozi kwa wakazi wa Ntube

23 May 2024, 5:15 pm

Picha ni Bustani ya mbogamboga ambayo ipo pembezoni mwa bwawa hilo ambapo wakulima hustawisha mbogamboga mbalimbali. Picha na Yussuph Hassan.

Bwawa Ntube ni bwawa ambalo limekuwepo katika mtaa huo kwa miaka mingi ambapo huhifadhi maji kwa mwaka mzima bila kukaua hivyo kuwa msaada kwa wakazi wa mtaa huo.

Na Mariam Kasawa.
Wakazi wa mtaa wa Ntube kata ya Nkuhungu wameiomba serikali iwasaidie kupata vifaa vya kisasa vya kilimo cha umwagiliaji pamoja na wataalamu wa kilimo ili waweze kunufaika na bwawa Mtube lililopo katika mtaa huo.

Ntube ni mtaa unaopatikana katika kata ya Nkuhungu iliyopo Jijini Dodoma katika mtaa huu linapatikana bwawa la asili ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo kwani linasaidia katika ufugaji wa samaki, kilimo cha mbogamboga , miti ya matunda pamoja na Mpunga.

Licha ya bwawa hilo kuwa na manufaa kwa akazi hao lakini bado wamekuwa wakipitia baadhi ya changamoto ambapo wanasema wanatamani kupata vifaa na mbegu za kisasa ili waweze kufanya kilimo chenye tija.

Sauti za wakulima.
Picha ni bwawa hilo ambalo lipo katika mtaa wa Ntube kata ya Nkuhungu. Picha na Yussuph Hassan

Nimezungumza na mwenyekiti wa Mtaa huo Bw. John Masaka anasema wanajitahidi kuimarisha ulinzi katika bwawa hilo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwao pia amewataka vijana kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili wajikwamue kiuchumi.