Dodoma FM

Maonesho ya wiki ya viwanda na biashara yazinduliwa Dodoma

22 May 2024, 9:10 am

Picha ni Mhe. Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar akifungua maonesho hayo. Picha na TanTradetz.

Wananchi wametakiwa kuwa na desturi ya kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda Nchini ili kukuza viwanda hivyo na uchumi wa nchi .

Na Mindi Joseph.
Serikali imetoa wito kwa wadau wa sekta ya Viwanda na Biashara kuzingatia mambo matatu ambayo ni utumiaji wa malighafi za ndani, kuajiri watanzania na kuwa na bidhaa zitakazohimili soko la ushindani ili kuunga mkono hatua mbalimbali inazozifanya katika kuondoa changamoto zinazoathiri ukuaji wa sekta hiyo.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Omar Said Shaaban amesema hayo leo wakati akifungua wiki ya Viwanda na Biashara katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Amesema duniani kote sekta ya viwanda ndio chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali na ni mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuongeza thamani ya malighafi,kutoa ajira kwa wananchi,kuongeza mapato ya serikali na kuboresha teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi na kuondoa umaskini nchini.

Sauti ya Mh,Omar Said Shaaban.
Maonesho ya Wiki ya Viwanda na Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma yakiwa yanaenda sambamba na usomaji wa Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara.Picha na TanTradetz.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Excaud Kigahe amesema maonyesho hayo ni sehemu ya kutoa elimu kuhusu wizara hiyo ili watanzania wajue kazi mbalimbali zinazofanywa na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi.

Sauti ya Mh. Excaud Kigahe

Kwa upande wake, Ofisa Habari Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Theresia Chilambo amesema lengo la ushiriki wao ni kutoa elimu kwa wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kuhusu masuala ya urasimishaji biashara na kueleza utaraitubu wa kujisajili Brela
Clip..Brela

Sauti ya Bi.Theresia Chilambo