Dodoma FM

Uhai wa viumbe hai unavyobebwa na uchavushaji

21 May 2024, 1:30 pm

Uwepo wa nyuki katika mazingira una jukumu muhimu katika kudumisha usawa wa ikolojia.Picha na You tube.
Nyuki wanachangia katika mzunguko wa rasilimali na kuchanganya vikundi vingine vya wanyama na mimea kwenye mnyororo wa chakula.

Na Mariam Kasawa.
Kwa mujibu wa watafiti wanasema kuwa asilimia 80 ya uchavushaji unaonaofanywa na nyuki ni muhimu kwa viumbe hai kwani pasipo uchavushaji hakuna maisha.

Mustakabali wa binadamu na mifumo ya ekolojia hutegemea uchavushaji takriban asilimia 80 ya spishi za mimea ya porini inayotoa maua hutegemea kabisa, au angalau kwa sehemu fulani, uchavushaji wa wanyama uchavushaji huchangia moja kwa moja kwa utoshelezaji wa chakula na ni muhimu katika kuhifadhi bayoanuai.

Hata hivyo, ufanyaji kilimo cha aina moja tu ya mimea na utumiaji mbaya wa dawa za kuulia wadudu ni tishio kubwa kwa vichavushaji kwa sababu hupunguza ufikiaji wa chakula na mahali pa kutagia, kuwapelekea kukumbana na kemikali hatari, na kudhoofisha mfumo wao wa kinga.

Wataalamu wanasema asilimia 80 ya uchavushaji hapa Duniani hufanywa na nyuki bila nyuki hakuna viumbe hai wanaoweza kuishi katika Dunia kwani uchavushaji huu hupelekea mazingira kuwa mazuri, upatikanaji mkubwa wa mazao ya shambani na matunda.

Nyuki ni muhimu kwa sababu ya jukumu lao katika uchavushaji Wanapokula nekta kutoka kwenye maua, poleni huambatana na miili yao na hii inasambazwa kwenye maua mengine wanayotembelea hii inachangia katika uzalishaji wa matunda, mboga, na mazao mengine, Hata hivyo, nyuki wamekumbana na tishio la kupungua kwa idadi yao katika miaka ya hivi karibuni Sababu za kupungua kwa nyuki ni pamoja na mabadiliko ya mazingira, upungufu wa malisho ya maua, matumizi ya dawa za wadudu katika mimea, pamoja na magonjwa.

Huyu hapa ni Mtafiti kutoka Taasis ya utafiti wa wanyamapori Tawiri akieleza jinsi Nyuki wanavyo saidia kuchavusha mimea na kuleta faida kubwa kwa viumbe hai.

Uwepo wa nyuki katika mazingira una jukumu muhimu katika kudumisha usawa wa ikolojia. Wanachangia katika mzunguko wa rasilimali na kuchanganya vikundi vingine vya wanyama na mimea kwenye mnyororo wa chakula.

Uwepo wa nyuki katika mazingira una jukumu muhimu katika kudumisha usawa wa ikolojia.Picha na You tube.

Mafunzo ya ufugaji wa nyuki wapole kwa wanafunzi hususani wanafunzi wa vyuo yanatajwa kuwa yataleta manufaa kwani yatapelekea wanafunzi hawa kujikita katika uuzaji wa mazao ya nyuki na kujikwamua kiuchumi lakini kwanza wanapaswa kuzingatia kutunza mazingira na kupanda miti.

Uharibifu wa mazingira, kama vile ukataji miti ovyo, uchomaji wa misitu, na mabadiliko ya matumizi ya ardhi, unaweza kusababisha upotevu wa malisho ya nyuki. Nyuki hutegemea aina mbalimbali za maua kama chakula chao. Wakati mazingira yanaharibiwa, mimea inapotea au inapungua, na hivyo nyuki wanakosa vyanzo vya chakula. Hii inaweza kuathiri sana afya na uhai wa makoloni ya nyuki.