Dodoma FM

Nishati ya jua mkombozi wa mkulima

17 May 2024, 11:48 am

Picha ni solar inayotumia nishati ya jua ambayo imefungwa shambani kwaajili ya umwagiliaji .Picha na Mindi Joseph.

Mradi huu unalenga kubadili tabia na Mtazamo kwa Wakulima kutumia nishatia ya jua katika shughuli za kilimo.

Na Mindi Joseph.
Matumizi ya nishati ya jua katika shughuli za Kilimo imetajwa kuwa Mkombozi kwa Wakulima kutokana na kuokoa gharama mbalimbali pamoja na kuwezesha uzalishaji wenye tija kwa msimu mzima.

Hizi ni sola ambazo wakulima wa kata ya Matumbulu wanatumia katika kilimo kwa ajili ya kumwagilia nyanya, vituguu, zabibu, mbogamboga na mazao mengine huku ikitajwa pia kusaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi..

Yohana Cheti ni mkulima wa nyanya amevutiwa na matumizi ya sola katika kilimo kwani ana chanzo kikubwa cha maji.

Bwana Festo Felix ni Meneja Shamba Don Bosco lilipo Miyuji Dodoma anasema kuna manufaa makubwa kwa mkulima kutumia sola katika kilimo endapo tu atatumia mitambo ya sola.

Sola mkulima ni mitambo ya kuaminika na ya gharama nafuu hususani vijijini Wakulima wa kata ya Matumbulu nimewauliza Je wamenufaikaje na matumizi ya Sola kwenye Kilimo.

Brian Ssenabulya ni Afficer Programme Taasisi ya African Center for Media Excellence ACME ambao wanatekeleza mradi huu kwa kushirikiana na chuo cha Don Bosco Bosco anasema matumizi ya sola katika kilimo inaongeza thamani katika kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Picha ni shamba la zabibu katika kijiji cha Matumbulu Jijini Dodoma ambalo ni moja ya matokeo ya kilimo cha umwagiliji kwa kutumia umeme jua.Picha na Mindi Joseph.