Dodoma FM
Sumukuvu hatari kwa usalama wa chakula
7 May 2024, 7:27 pm
Kulingana na shirika la Afya Duniani (WHO), sumu kuvu huharibu karibu asilimia 25 au zaidi ya chakula kinachozalishwa duniani kila mwaka.
Na Mindi Joseph.
Tatizo la Sumukuvu limetajwa kuhatarisha usalama wa chakula hivyo kuiweka idadi kubwa ya walaji kuwa katika hatari.
Sumu kuvu ni familia ya sumu zinazozalishwa na kuvu zinazopatikana katika mimea inayopandwa kama vile mahindi, karanga na pamba na huathiri mimea iliyoko shambani wakati wa kuvuna na kuhifadhi mazao.
Mratibu wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania Clepin Josephat anasema athari za sumu kuvu kwa Afya ya binadamu ni kubwa.
Ameongeza kuwa katika uchumi madhara ya sumukuvu ni makubwa hivyo wanawekeza nguvu kuhakikisha chakula kinachozalishwa ni salama.