Kaulimbiu ya TEF yamkosha Naibu waziri mkuu
30 April 2024, 6:45 pm
Hapo jana April 29 Jukwaa la wahaariri TEF lilizindua mkutano wa 13 hapa jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Dotto Biteko .
Na Mariam Kasawa.
Kaulimbiu ya mkutano wa jukwaa la wahariri inayosema Uandishi wa habari kuhamasisha matumizi ya Gesi kulinda misitu inatajwa kuchochea matumizi ya nishati safi ili kulnda mazingira.
Akiongea katika mkutano huo Waziri Biteko amesema kuwa kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa, kwa Ripoti ya tatu ya mwaka 2019.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameomba wahariri kutumia kalamu zao katika kuwatoa hofu wananchi juu ya matumizi ya gesi kwani watu bado wanahofu na kuwapongeza kutumia akili kubwa katika kuipata kaulimbiu hii kwani anaamjni wataitendea haki.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bwana Deodatus Balile wakati akisoma Risala yao amesema kuwa wao kama Wahariri wanatamani kuona mchango wa rasilimali gesi katika uchumi wa nchi yetu na watu wake.
Hadi kufikia 2015, uzalishaji wa mkaa duniani ulikadiriwa kuwa tani milioni 52 kwa mwaka, na kati ya hizo tani milioni 32.4 zinazalishwa Afrika, ambapo asilimia 42 ya tani hizo zinazalishwa katika ukanda wa Afrika Mashariki unaohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi. Afrika Magharibi inazalisha asilimia 32, Afrika ya Kati (12.2), Kaskazini (9.8) na Kusini mwa Afrika ni asilimia 3.4.Takwimu hizi zinaashiria hatari kubwa. Misitu inateketea katika ukanda wetu.”