Ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato wafikia 54%
24 April 2024, 6:16 pm
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alieleza kuwa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato umefikia asilimia 54.1 kwa sehemu ya kwanza.
Na Mindi Joseph.
Ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato umefikia asilimia 54 na asilimia 21 katika miundombinu ya barabara huku ukitajwa kuchangia kukua kwa kata ya msalato.
Ujenzi huo unajumuisha ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara za maungio na barabara za kuingia na kutoka kiwanjani hapo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Msalato, Nsubi Bukuku.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kupitia kwa Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Mussa Mbura anasema ujenzi wa uwanja huo unatarajiwa kufanyiwa majaribio ya urushaji ndege mwezi Oktoba 2024 na ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika mwaka 2025.