Jamii yaaswa kuzingatia matumizi sahihi ya mitandao
27 March 2024, 6:14 pm
Ulimwengu kwa sasa umeshuhudia ukuaji mkubwa wa matumizi ya teknolojia na pia intaneti Lakini watumiaji wengi wa teknolojia hizi wamekua katika hatari ya kuingia katika matumizi mabaya ya teknolojia hii kutoka na wizi na vitendo vya udhalilishaji vinavyoweza kutokea kupitia mitandao.
Na Fred Cheti.
Jamii imetakiwa kuzingatia matumizi sahihi na kuwa makini na mitandao ili kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na wizi vinavyoweza kujitokeza endapo mitando hiyo haitotumiwa kwa uangalifu.
Hayo yameelezwa na Meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kati(TCRA) Mhandisi Asajile John wakati akifanya mahojiano na Dodoma fm redio katika kipindi cha Dodoma Live kuhusu namna Sahihi na salama ya matumizi ya mitandao .
Dodoma Tv imefanya mazungumzo na baadhi ya wananchi jijini hapa kuhoji je jamii ina uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ?na nini kifanyike ili kutoa uelewa zaidi?