Elimu ya utunzaji Mazingira yawanufaisha wanafunzi
27 March 2024, 5:38 pm
Wadau wa mazingira wanasema vijana wanapaswa kutambua kwamba jukumu la utunzaji wa mazingira ni la kila mmoja katika jamii hivyo ni vema washiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira.
Na Mariam Kasawa.
Elimu ya utunzaji mazingira na kilimo inatajwa kuwanufaisha wanafunzi na kuwajenga kuishi katika jamii kwa usahihi pindi wanapo hitimu masomo yao .
Baadhi ya shule licha ya kuwafundisha wanafunzi masomo mbalimbali lakini pia wamejikita kuwafundisha wanafunzi utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti, maua na bustani ndogondogo za mbogamboga elimu inayo onesha kuwafaa zaidi wanafunzi.
Elimu hii itasaidia pia ni msaada kwa jamii zinazo wazunguka wanafunzi hawa , kwani wanafunzi hawa wako tayari kutoa elimu hii na kufanya kile walichojifunza katika maeneo yanayowazunguka.
Shule ya Sekondari Chamwino ni moja kati ya shule ya mfano kwani imefanikiwa kuboresha mazingira yake kuwa ya kuvutia kwa kupanda miti, maua na bustani za mbogamboga mazingira ya shule hii yananivutia na kunifanya nitamani kukutana na mwalimu wa mazingira hapa akanieleza siri ya mafanikio yao.
Wanafunzi nao wanaeleza faida wanayoipata katika elimu ya urunzaji wa mazingira na kilimo cha mbogamboga na matunda.