Soko kuu Majengo lafanikiwa ukusanyaji taka.
15 March 2024, 6:40 pm
Wananchi wanahimizwa kuendelea kuweka mazingira katika hali ya usafi huku wakitakiwa kufahamu kuwa kuweka takataka chini ni kosa kisheria.
Na Mariam Kasawa.
Soko Kuu la majengo jijini Dodoma limefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika zoezi la ukusanyaji yaka hali inayopelekea mazingira kuwa safi wakati wote.
Baadhi ya wafanyabishara katika soko hilo wanasema hali ni tofauti na hapo awali kwani hakuna tena mrundikano wa taka wao hulazimika kulipa ada ya taka ambayo ni shilingi 1000 kila wiki na taka hukusanya kila siku na kupelekwa eneo husika.
Kwa mujibu ya sheria ya mazingira kifungu cha 117 inasema mamlaka ya serikali za mitaa itahakikisha kwamba mashimo ya taka na maeneo yaliyotengwa mahsusi na viwanda kwaajili yya kukusanyia taka yanawekwa katika hali ya usafi na yanalindwa dhidi ya nzi , wanyama na viumbe wanaokula mizoga.
Wafanyabiashara wa eneo hili wanatamani kuwekewa vifaa vya kisasa vya kutunza taka kila baada ya hatua ili kuepuka kuweka taka kwenye ndoo au mifuko ambayo hujaa haraka na kusababisha taka kuzagaa.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usafi na uondoshaji wa taka katika Jiji la Dodoma Bw. Dikson Kimaro yeye anasema wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya utunzaji mazingira mara kwa mara hususani sokoni ili watu waepuke kutupa taka ovyo.