Wakulima waomba elimu ya mbegu bora mapema kabla ya msimu wa kilimo
26 February 2024, 5:38 pm
Wakulima wanakumbushwa kuendelea kutumia mbegu bora ili waweze kupata mavuno mazuri pia wanashauriwa kukagua mbegu hiwa kabla ya kuzinunua ili kuthibitisha alama ya ubora.
Na Mariam Kasawa.
Wakulima wameomba kupatiwa elimu ya mbegu mapema kabla ya msimu wa kilimo kuanza ili waweze kuepukana na athari za kupanda mbegu ambazo hazina manufaa kwao.
Ni msimu wa kilimo ambapo tayari maeneo mengi ya mkoa wa Dodoma wakulima wamesha otesha mbegu shambani huku wengi wakisema hiki ni kipindi cha palizi msimu wa kuua magugu shambani.
Lakini baadhi ya mashirika wakiwemo Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI)hayajawasahau wakulima bado wanawatembelea na kuwapatia elimu ya uchaguzi sahihi wa mbegu zinazo faa kwa kilimo, licha ya elimu hiyo haya hapa ni matamanio ya wakulima kutoka kijiji cha Mkoka kilichopa wilayani Kongwa mkoani hapa.
Afisa kilimo kutoka kijiji cha Mkoka Bw.Marcelin Chingilile anasema wanajitahidi kuwatembelea wakulima na kuwapatia elimu ya matumizi ya mbegu bora.
Ni faida gani hasa anapata mkulima pale anapo amua kuchagua mbegu bora huyu hapa Bw. William Hilonga Mkaguzi wa mbegu kutoka Tosk akiwafunda wakulima wa kijiji cha Mkoka.