Wananchi wakosa elimu ya kutosha utunzaji wa mbegu
23 February 2024, 5:10 pm
Wakulima wanashauriwa kutumia mbegu bora kwa kununua mbegu katika duka lililosajiliwa na TOSCI ili kusaidia kubaini nani anayesambaza mbegu zisizo na ubora na kurahisisha namna ya kutatua changamoto itakayokuwa imejitokeza.
Na Mindi Joseph.
Uhifadhi sahihi wa mbegu umetajwa kuwa changamoto na kuchangia kutunza mbegu sehemu isiyokuwa sahihi hivyo kusababisha kupotea kwa ubora na uotaji wa mbegu.
Mkaguzi wa mbegu kutoka Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania(TOSCI) Dickson Manyama ameyabainisha hayo.
Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Kudhibiti Ubora wa Mbegu yaliyofanyika jijini Dodoma yanalenga kufikisha ujumbe lengwa kwa wakulima.
Wakulima wanashauri kutumia mbegu bora kwa kununua mbegu katika duka lililosajiliwa na TOSCI ili kusaidia kubaini nani anayesambaza mbegu zisizo na ubora na kurahisisha namna ya kutatua changamoto itakayokuwa imejitokeza.