Tabia bwete yatajwa chanzo cha ugonjwa wa kisukari
15 February 2024, 5:01 pm
Ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na mtindo mbovu wa maisha ni muhimu kufanya mazoezi ya wastani ya dakika 35 hadi 45 mara kwa mara.
Na Mindi Joseph.
Imeelezwa kuwa tabia Bwete ikiwemo kutofanya mazoezi unene uliopitiliza,kula vyakula vya wanga na mafuta kwa wingi ni chanzo cha ugonjwa wa Kisukari.
Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoua kimya kimya katika kundi hili la magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Watu milioni 285 Duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni.
Kuepuka uvutaji wa singara na unywaji wa pombe kupita hatari inasaidia kukabiliana na ugonjwa huo
Alemiana Alex ni Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma anashauri nini kifanyike.
Nao baadhi ya wananchi wamezungumzia uelewa wao kuhusu Ugonjwa wa Kisukari.