Wafanyabiashara Sabasaba washukuru kuboreshewa miundombinu ya soko
13 December 2023, 8:59 pm
Soko la sabasaba ni miongoni mwa masoko makubwa na maarufu katika jiji la dodoma ambapo kwa mujibu wa baadhi ya wakaz wa jiji la dodoma wanasema kuwa soko hili linasifika kwa kuuzwa bidhaa za mbogamboga na matunda kwa bei rahii zaidi ukilinganisha na msoko mengine.
Na Thadei Tesha.
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la sabasaba Jijini Dodoma wameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu katika soko hilo kwani ilikuwa ikiwapa changamoto hasa wakati wa kipindi cha mvua.
Hili ni soko la sabasaba lililopo Jijini hapa ambapo awali lilikuwa na changamoto kubwa hususani katika kipindi cha mvua lakini kwa sasa hali ni tofauti, baadhi ya wafanyabiashara katika soko hili wanaeleza namna maboresh hayo yalivyosaidia kubadilisha taswira ya soko hilo.
Pamoja na kufanyika kwa maboresho hayo dodoma tv imewauliza baadhi ya wafanyabiashara kuhusiana na hali ya bei za bidhaa hususani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu hali ipoje?