Mlowa barabara wadai wizi wa mifugo unarudisha nyuma maendeleo yao
19 November 2023, 11:45 am
Wimbi la wizi wa mifugo limerejea kwa kasi mkoani hapa baada ya kuwepo utulivu wa zaidi ya miaka 17.Picha na Muungwana blog.
Hata hivyo Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya jeshi la akibaa lengo ikiwa ni kuimarisha ulinzi kwa jamii husika.
Na Victor Chigada
Imeelezwa kuwa wizi wa mifugo kwa baadhi ya vitongoji katika Kata ya Mlowa Barabarani bado unaendelea licha hatua mbalimbali kuchukuliwa.
wananchi wa kijiji cha Mloda wamesema kuwa changamoto hiyo imekuwa ikiwarudisha nyuma kimendeleo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Adamu Philimini amekiri uwepo wa wimbi la wizi licha ya juhudi za ulinzi wanazo zichukua lakini baadhi ya wenyeji wamekuwa wakishirikian na wageni kufanya vitendo hivyo
Naye Diwani wa Mlowa Barabarani Bw.Anjero Lucas amethibitisha uwepo wa changamoto hiyo ya wizi wa mifugo licha ya kufanikiwa kupunguza adha hiyo
Lucas ameongeza kuwa kwasasa uwepo wa kituo cha polisi ndani ya Kata yao imekuwa chachu ya kupunguza changanoto kwa wafugaji