Jamii yatakiwa kushiriki kutokomeza rushwa ya ngono
1 November 2023, 11:21 am
Rushwa ya ngono inaweza kusababisha athari kubwa kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Na Aisha Alim.
Jamii imetakiwa kushirikaiana katika kuhakikisha vitendo vya rushwa ya ngono makazini vinatokomezwa kwani ni miongoni mwa vitendo vya ukatili vinavyomnyima mtu haki yake ya msingi.
Hayo yamesemwa na Inspekta Jelda Uyangi kutoka dawati la jinsia mkoa wa Dodoma katika mahojiano maalum na kituo hiki.
Amesema kuwa rushwa ya ngono inaweza kusababisha athari kubwa kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla endapo jamii haitashiriki kutokomeza vitendo hivyo .
Aidha baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wameelezea mtazamo wao juu ya suala hili katika jamii huku wakiwataka wanaofanya vitendo hivi kuacha.
Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya Mwaka 2007; Rushwa ya Ngono ni kitendo anachofanya Mtu mwenye Mamlaka, katika kutekeleza Mamlaka yake kudai Ngono au upendeleo wa aina yoyote kutoka kwa Mtu kama kishawishi cha kumpatia Ajira, Cheo, Haki, Fursa au upendeleo mwingine.