Wakazi wa Handali walalamika kukosa maji safi na salama
16 October 2023, 6:44 pm
Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wapo kwenye mpango wa bajeti katika kuhakikisha miundombinu ya maji katika kijiji cha Handali inafufuliwa.
Na Mindi Joseph.
Kusimama kwa Mradi wa Maji unaogharimu zaidi ya Milioni 600 katika kijiji cha Handali Wilayani Chamwino imechangia wakazi wa eneo hilo kutumia maji yasiyo safi na salama.
Dodoma Tv imefanikiwa kufika katika Mradi huo na kushuhudia baadhi ya adha wanazopitia wananchi wa kijiji hicho ambapo inawalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi na salama.
Tumezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ambaye ni Diwani wa Kata ya Idifu Samwel Kawea Kujua ni hatau zipi halmashauri wanachukua kuhakikisha wananchi wa kijiji hicho wanafanikiwa kupata huduma ya maji safi na salama.
Katika kutatua changamoto hiyo ya Maji, Jumuiya ya watumiaji maji imeanzishwa katika Kijiji cha Handali .