Dodoma FM
Usimamizi mbovu wapelekea biashara nyingi kufa
27 September 2023, 4:22 pm
Usimamizi wa biashara nyingi umekuwa ni changamoto na sababu kubwa inayochangia kuanguka kwa asilimia kubwa ya biashara hizo.
Na Mindi Joseph.
Usimamizi wa Biashara kwa wafanyabiasha imetajwa kuwa bado ni changamoto inayochangia kuanguka kwa asilimia kubwa ya biashara.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Mikopo ya EFL Profesa Goodluck Urassa amesema wajasiriamali wengi wanaanza biashara lakini hawasimamii inavyopaswa.
Ameongeza kuwa usimamizi mzuri wa biashara unajumuisha mambo mengi yakiwemo, udhibiti wa mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa au huduma kwenye biashara, udhibiti wa mali na rasilimali za biashara ukiwemo muda pamoja na udhibiti wa manunuzi na bajeti..