Dodoma FM
Vilindoni yahitaji uzio kuepuka migogoro na wananchi wa jirani
12 September 2023, 3:51 pm
Hali ya usalama imekuwa Ndogo kwa wanafunzi kutokana na shule hiyo kukosa Uzio hali inayosababisha baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la shule hiyo.
Na Mindi Joseph.
Ukosefu wa uzio katika shule ya Msingi vilindoni imeelezwa kuchangia mwingiliano wa shughuli za kijamii ikiwemo ufugaji.
Mifugo imekuwa ikikatiza katika eneo hilo la shule na kusababisha migogoro baina ya uongozi wa shule na wafugaji.
Mwalim Mkuu wa shule ya msingi Vilindoni Dorotea Mdushi anasema.
Wananchi wanasema changamoto ya kukosekana kwa uzio imechangiwa na wananchi kuvamia mipaka ya shule.