Tume ya haki za binadamu yabaini maeneo yanayoongoza utumikishaji watoto
13 June 2023, 2:39 pm
Maadhimisho ya siku ya kupinga ajira kwa watoto hufanyika june 12 kila mwaka na mwaka huu maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kaulimbiu isemayo haki ya jamii kwa wote. Kukomesha ajira ya watoto.
Na Pius Jayunga.
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imebaini uwepo wa maeneo yanayoongoza kwa utumikishaji mkubwa wa watoto nchini ikiwemo shughuli za kilimo, uchimbaji madini migodini pamoja na kazi za ndani.
Makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Mohamed Khamis Hamad amebainisha hayo wakati akizungumza na wandishi alipokuwa akitoa tamko la tume ya haki zabinadamu na utawala bora katika kuadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto, maadhimisho ambayo hufanyika ifikapo Juni 12 kila mwaka.
Aidha tume hiyo imetoa mapendekezo mbalimbalui ikiwemo serikali kuendelea na uhamasishaji wa hatua za kimataifa kufikia haki ya jamii na kuondoa ajira kwa watoto.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wakawa na maoni tofuati juu ya uwepo wa maadhimisho ya siku ya kupinga ajira kwa watoto huku wakisisitiza wazazi kutimiza jukumu la malezi kwa watoto.