Wanawake, vijana watakiwa kubadili mitazamo na kushiriki katika sekta ya kilimo
24 May 2023, 7:17 pm
Jukumu kubwa la taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masoko ya kilimo AMDT ni kuwezesha na kuboresha mabadiliko makubwa ya kimkakati kwenye mifumo ya masoko ya sekta za kilimo.
Na Mindi Joseph.
Vijana na wanawake wametakiwa kubadili mitazamo na kushirikiana na serikali ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na makamu mwenyekiti kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mh. Mariam Ditopile katika mdahalo wa wanawake vijana na uongozi kwenye sekta ya kilimo na biashara.
Amesema vijana na wanawake wana wajibu wa kutumia muda na kuwekeza katika kilimo kwa ufanisi mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi.
Kwa upande wao vijana walioshiriki katika mdahalo huo wamesema uwepo wa wanawake na vijana katika kilimo ni muhimu.
Meneja mwandamizi Jinsia, Vijana na Mazingira ya Biashara Mary Kalavo kutoka taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masokoya kilimo AMDT amesema mdahalo huo unalenga kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Kilimo.