Tume ya haki za binadamuyatangaza kuanza uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa UDOM
10 May 2023, 6:34 pm
Kwa Mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha sheria ya tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora sura ya 391 tume inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wake wenyewe juu ya malalamiko yanayoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora pasipo kusubiri kuletewa malalamiko.
Na Seleman Kodima.
Tume ya haki za Binadamu na utawala Bora imetangaza kuanza Uchuguzi wa kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma Bi Nusura Hassan Abdallah ambaye alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya faraja mkoani Kilimanjaro.
Taarifa ya tume ya haki za Binadamu na utawala bora iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa tume ya hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema kwa kipindi cha hivi karibuni tume ya haki za Binadamu na utawala bora imeona katika vyombo vya habari zikihuisha ajali ya Naibu waziri wa Tamisemi Dkt Festo Ndugange na kifo cha Nusura Abdallah .
Jaji Mstaafu Mwaimu amesema taarifa hizo za vyombo vya habari zimeoneakna kukinzana kutokana na taarifa zilizotolewa na jeshi la Polisi,Chuo kikuu cha Dodoma , hospitali ya Faraja iliyopo himo mkoani Kilimanjaro na taarifa za wananchi kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha Jaji Mstaafu Mwaimu amesema tume inapoona kumetokea mashaka kutoka kwa wananchi kuhusu jambo lolote linaloashiria uvunjwaji wa haki za binadamu au mashaka ya haki kutokutendeka ina mamlaka ya kufanya uchuguzi juu ya jambo hilo.
Hivyo amesema kuwa mujibu wa katiba na sheria za tume wana jukumu la kutetea na kulinda haki za binadamu nchini.
Pamoja na hayo amesema tume imeazimia kufanya uchuguzi wake huru kwa madhumuni ya kubaini ukweli kuhusu matukio hayo.