Kamati ya kuduma ya bunge ya maji na mazingira yatembelea bwawa la mtera
8 May 2023, 3:53 pm
Mradi wa Maji mtera unategemewa kuongeza maji na kufika jumla ya lita milioni 201 ambazo zitaweza kutumika kwa miaka 13 ijayo jijini Dodoma.
Na Seleman Kodima.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira pamoja na wataalamu kutoka wizara nne wametembelea bwawa la mtera ikiwa ni sehemu ya kujiridhisha na mpango wa haraka wa wizara ya maji wa kutoa maji katika bwawa hilo na kulete jijini Dodoma .
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe .Jackson Kiswaga kutembelea eneo la bwawa la mtera na kujionea hali halisi ya mpango huo ambapo unatarajiwa kuwa sehemu ya kujazilisha maji katika jiji la Dodoma na kuongeza hali ya uzalishaji wa maji .
Akizungumza hapo jana Mhe Kiswaga amesema kuwa licha ya kufanya ziara hiyo wamepata nafasi ya kusikiliza wataalamu ambapo waliambatana nao kuhusu mradi huo na kamati hiyo wataenda kukaa ili waweze kutoa majibu ya sahihi juu ya mpango wa mradi wa maji mtera.
Aidha ametoa ushauri kwa wataalamu wa mazingira kuhakikisha wanasimamia sheria ili kuepusha wananchi ambao wamekuwa wakivamia eneo la bwawa hilo na kuendesha shughuli za kilimo hali ambayo inahatarisha ustawi wa maendeleo wa bwawa la mtera.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso amesema mradi wa maji mtera ni miongoni mwa mikakati ya wizara ya maji ya kuhakikisha wanaendelea kusongeza huduma ya maji karibu kama ulivyompango wa serikali ya awamu ya sita .
Mhe Aweso amesema mahitaji ya maji kwa mkoa wa Dodoma lita milioni 133 ambapo kwa sasa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) wanazalisha lita milioni 67 huku pungufu ni Lita milioni 65 .
Hata hivyo Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji inaendelea na hatua mbalimbali ikiwemo kupata ushauri wa Mtaalamu mshauri ili maamuzi yatakayo fanyika yasiathirii shughuli nyingine za kijamii.