Hivi ndivyo hali ilivyo katika eneo la kimbinyiko
29 March 2023, 5:56 pm
Madereva pamoja na wajasiriamali katika eneo la kimbinyiko jijini Dodoma wameiomba serikali kutenga eneo maalum kwa ajili ya kupakia abiria kutokana na eneo hilo.
Na Thadei Tesha.
Baadhi ya madereva pamoja na wajasiriamali katika eneo la kimbinyiko jijini Dodoma wameiomba serikali kutenga eneo maalum kwa ajili ya kupakia abiria kutokana na eneo hilo kuwa na msongamano mkubwa hasa wakati wa asubuhi.
Dodoma FM imefika katika eneo hilo na kukuta shughuli za kupakia abiria pamoja na biashara ndogondogo zinaendelea na baadhi ya watumiaji wa eneo hilo wakazungumzia hali ilivyo kwa sasa?
Kwa upande wao abiria waliopo katika eneo hili wanasema eneo hilo limekuwa na changamoto kubwa kutokana na kukaa muda mrefu wakisubiri usafiri tofauti na ilivyokuwa katika kituo cha sabasaba huku wafanyabiashara wadogo wakisema kuwa kwao inapelekea kutembea muda mrefu kutafuta wateja.
Kwa mujibu wa madereva pamoja na watumiaji wa eneo hilo wanasema Baada ya kuhamishwa kwa kituo cha daladala cha sabasaba eneo hili limekuwa na msongamono mkubwa kwani abiria kutokea maeneo ya sabasaba hufika hapa kwa ajili ya kusubiri usafiri huo?