Wakazi wa Mpwapwa watakiwa kuendelea kuchangamkia fursa ya mikopo
24 March 2023, 2:40 pm
Amewataka wananchi hao kuendelea kuwaona wataalamu wa mikopo na Wachumi kwaajili ya kupata elimu zaidi kuhusu mikopo.
Na Fred Cheti.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe. Sophia Kizigo amewataka vijana,wanawake na wenye ulemavu kuendelea kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halamshauri ili iwakwamue kiuchumi.
Mhe Kizigo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo baada ya zoezi la utaoji wa mkopo wa shillingi milioni 90 kwa makundi hayo na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kwa mwaka huu wa fedha katika halmshauri hiyo kufikia milioni 134 huku akivitaka vikundi hivyo kuchukua mikopo mikubwa ili ilete tija zaidi.
Aidha Mhe Kizigo ametoa ushauri kwa makundi hayo kutosita kuona wataalamu wa masuala ya mikopo na uchumi ili wawapatie elimu ya namna nzuri ya kuitumia mikopo hiyo ili iwaletee manufaa na waweze kuirudisha kwa wakati.